banner

Saturday, July 29, 2017

Agizo la DC Mjema kwa askari wa usalama barabarani

Agizo la DC Mjema kwa askari wa usalama barabarani


Mkuu wa wilaya ya ilala Mh Sophia Mjema akipiga kiki pikipiki, katika hafla ya madereva wa bodaboda iliyoandaliwa kwaajiri ya kumshukuru Rais Dkt Magufuli kwa  kuunga mkono juhudi  zake katika kutatua changamoto za watanzania.leo jijini Dar es salaam.



Askari wa usalama barabarani wilayani Ilala Mkoani Dar-es-salaam wametakiwa  kuacha kuwadhalilisha vijana wanaofanya biashara ya bodaboda na badala yake wazingatie sheria,kanuni na taratibu.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema ametoa wito huo leo wakati akipokea maandamano ya bodaboda  wanaounga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kutatua changamoto za Watanzania na kuongeza kuwa vijana hao wanatakiwa kupewa ushirikiano wa kutosha ili waweze kufanya kazi zao za kujitafutia kipato.

Mapema wakisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya bodaboda hao wamemueleza namna ambavyo wamekuwa wakinyanyaswa na kudhalilishwa na askari wa usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali iwaruhusu kufanya kazi mpaka maeneo ya katikati ya jiji.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala ACP. Lucas Mashishanga amewataka bodaboda hao kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akipiga marufuku ulinzi shirikishi kuwasumbua bodaboda hao na kwamba wamejipanga kufanya kazi kwa pamoja.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search