banner

Friday, August 4, 2017

Mrisho Mpoto atua Nane Nane Arusha 'watanzania wenyewe ndio watalii wa kweli

Mrisho Mpoto atua Nane Nane Arusha 'watanzania wenyewe ndio watalii wa kweli

Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto ambaye pia ni Balozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  baada ya wiki hii kuachia wimbo wake mpya ‘Kitendawili' akiwa amemshirikisha muimbaji Kassim Mganga, Ijumaa hii ametua jijini Arusha kwaajili ya maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za 'Nane Nane’ mwaka 17 Kanda ya Kaskazini.
 Mshairi huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na utamaduni wa Tanzania, amewataka wakulima pamoja na watanzania nchini kutembelea hifadhi ya Ngorongoro ili kujifunza na kuona mambo mengi ambayo hayapatikani sehemu yoyote zaidi ya Tanzania.
Bendi ya Mpoto imetoa burudani pamoja na elimu kwa umati mkubwa wa watu uliojikusanya katika banda hilo huku burudani hiyo ikiambatana elimu kuhusu hifadhi hiyo.  
    
Akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza katika maonyesha hayo, Mpoto amewaka wananchi kujiwekea utamadani wa kutembelea hifadhi za taifa kwa kuwa ni sehemu ambao inaweza kuwajenga watu na kufahamu mambo mengi kuhusu rasilimali walizonazo.
"Hii ni Nane Nane na tukizungumzia Nane Nane ni wakulima au mazao ya kilimo yanayozalishwa ndani na kusindikwa kuwa bidhaa. Lakini mimi kama balozi wa Hifadhi ya Ngorongoro ndani ya siku hii muhimu kwa taifa letu nikiwa pamoja na hifadhi ya Ngorongoro tumekuletetea ofa ya kwenye Ngorongoro katika msimu huu wa Nane Nane kwa kiwango cha chini zaidi ili kila mtu aende kujionea maajabu, ni shilingi 50,000 tu ukiwa hapa Arusha mjini itaweza kukupeleka Ngorongoro hiyo hiyo usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, kiingilio pamoja na kupewa mtu ambaye atakuongoza kukupeleka katika vivutio vyote  vya Ngorongoro,” alisema Mpoto. 
Aliongeza, "Kuna wakati tunaona mambo ni magumu unahitaji bajeti kubwa kumbe sio, ukiwa na pesa kama hiyo unafurahi kabisa,tena watoto ni tsh 20000 tu sasa kazi ni kwako kuna siku tatu kuanzia tarehe 6,7 na 8,”

Kwa upande wa Afisa Hifadhi ya Ngorongoro, Peter Makutian . amesema Ngorongoro bado inahitaji watanzania wengi kwa kuwa ina vitu vingi ambavyo kila mtanzania anahitaji kuvijunia huku akieleza kituko kipya cha hivi karibuni kilichotokea kwenye hifadhi hiyo baada ya Simba kuonekana akimnyonyesha mtoto wa Chui.
"Ngorongoro kuna mambo mengi sana kama mlivyosikia hivi karibuni kuna Simba ameonekana akimnyonyesha mtoto wa chui, hiyo ni kweli imetokea ni kitu ambacho hakijawahi kutokea na kuonekana duniani kwa sababu ni wanyama ambao kila mmoja ana mfumo wake wa maisha, kwa hiyo mnakaribishwa kushuhudia hilo,” alisema.  

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search