banner

Saturday, July 29, 2017

RC Makonda ndani ya Komaa Concert ya E FM

RC Makonda ndani ya Komaa Concert ya E FM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameongoza maelfu ya watanzania waliojitokeza viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe, kuhudhuria tamasha la Komaa (KOMAA CONCERT) lililoandaliwa na chombo cha habari cha E FM.

RC Makonda amewapongeza E FM kwa maandalizi ya Tamasha hilo ambalo limewakutanisha watanzania wa hali ya chini kutoka maeneo mbalimbali ambao wamepata fursa ya kushuhudia Tamasha hilo ambalo limewahusisha wasanii mbalimbali wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya, singeli na Hip Hop.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewataka E FM kuendelea kuongeza masafa mikoa mingine ili watanzania wengi waendelee kuipata huduma yao iliyo bora.
RC Makonda na Msanii Snura Tamasha la Komaa Concert

Mkuu  wa Mawasialiano wa Kituo cha EFM Redio  Denis Sebo akizungumza na wananchi waliohuzulia Tamasha la Komaa Concert.
Msanii Harmonize akitumbuiza katika Tamasha la Komaa Concert
Msanii Harmonize

Msanii Rubby akitumbuiza katika Tamasha la Komaa Concert


Hitmaker wa Libebe Beka Flavour akitumbuiza Tamasha la Komaa Concert


Hit Maker wa Pepeta Chin Beese katika Tamasha la Komaa (Komaa Concert)


Msanii wa Hip Hop Country Boy akitumbuiza katika Tamasha la Komaa Concert
Msanii wa Hip Hop Witnesz Kibonge Mwepec 









Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search