banner

Friday, August 18, 2017

Wema bado ngoma nzito mahakamani

Wema bado ngoma nzito mahakamani

Uamuzi wa kupokea au kutopokea kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania 2006 na muigizaji Wema Sepetu utatolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwisho wa mwezi huu.


Hakimu Mkazi Mkuu mahakama ya Kisutu, Thomas Simba amewaambia mawakili upande wa utetezi na serikali kuwa uamuzi huo ulipaswa autoe leo, lakini bado kuna tafiti ambazo anazifanya na hazijakamilika hivyo wanapswa kurejea tena mahakamani  Agosti 31,2017.

Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13, 2017
Wema Sepetu wenzake wawili wanakabiliwa na shtaka la kukutwa na dawa za kulevya huku tayari vipimo kutoka ofisi ya Mkemia wa Serikali vikionyesha kwamba mkojo uliopimwa unaonyesha kuwa na vimelea vya bangi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search