banner

Thursday, August 31, 2017

DC atao agizo hili kwa makanisa yanayopiga muziki na kufanya ibada masaa 24

DC atao agizo hili kwa makanisa yanayopiga muziki na kufanya ibada masaa 24

Mkuu wa wilaya ya Musoma mkoani Mara, Dkt. Vincent Anney ameibuka na kupiga marufuku upigwaji wa muziki holela pamoja na baadhi ya makanisa yanayofanya ibada kwa masaa 24 na kusema wanavunja haki za watu wengine. 

Dkt. Vincent Anney amewataka watu wa makanisa kuwasilisha kwake ratiba yao ya ibada kwa kuwa wana haki ya kuabudu na amewataka pia wanaotaka kufanya mikutano ya injili lazima wapate kibali kwa ajili ya mikutano hiyo. 

"Wana haki ya kuabudu wawasilishe ratiba ya zao za kuabudu katika ofisi yangu ya Mkuu wa Wilaya wakitaka kufanya mikutano ya nje wapate kibali, mimi nimepiga marufuku muziki wa holela uwe wa dini wa kawaida, muziki wa dansi ambao watu wanapiga masaa 24 kuna haki za raia wengine vinavunjwa na hao wenye makanisa ambao wanahubiri masaa 24" alisema Mkuu wa Wilaya ya Musoma 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search