banner

Friday, March 1, 2024

JE UNAIFAHAMU HISTORIA YA PICHA HII YA RAIS MWINYI NA NGULI POP MICHAEL JACKSON

JE UNAIFAHAMU HISTORIA YA PICHA HII YA RAIS MWINYI NA NGULI POP MICHAEL JACKSON

Miongoni mwa Picha maarufu mitandaoni ni hii ya Mfalme wa Pop marehemu #MichaelJackson na Hayati Ali Hassan Mwinyi ambaye hapo alikuwa Rais wa Tanzania.



Unafahamu chochote juu ya Picha hii yenye thamani? Karibu tukujuze; Michael Jackson aliitembelea Tanzania Februari 1992. Alitua uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam kwa ndege yake mwenyewe akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Benzi iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, ambapo sasa ni Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam.


Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani kama ‘Mfalme wa Pop’ hadi anakufa mwaka 2009, alifika nchini akiwa balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Hassan Diria. Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na Rais Ali Hassan Mwinyi (Picha Juu)


Kesho yake alitembelea shule maalum ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyopo Sinza. 

Ndege yake iliyokuwa na watu takriban 60 ilishindwa kwenda mbugani Ngorongoro alikotaka kwenda. Na yeye alikuwa hawezi kupanda ndege ndogo, hivyo akaishia Dar es salaam. Sehemu nyingine aliyotembelea na kuacha gumzo ni jumba la sinema la Empire mtaa wa Azikiwe ambako aliingia katika duka la kukodi mikanda ya sinema. Naye alibeba mikanda kama 10 hivi ya vikatuni, ikiwemo ya Tom and Jerry.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search