banner

Saturday, November 4, 2023

NITAWATAJA MAFISADI JUMATATU

 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ametoa ahadi ya kuwataja wote walioko nyuma ya ufisadi wa Kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Standard Gauge Railway (SGR), Jumatatu ya November 06,2023. 



Mbunge Ole Sendeka ametoa kauli hiyo leo November 4 2023 wakati akichangia mjadala wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) na Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


“Mimi nigekuwa Waziri miezi sita hii hakuna ambaye angebaki aliyetuhumiwa kwenye ufisadi kwenye Wizara yangu lakini nataka niwaambie wako Watu wamefisadi kuanzia wa IPTL leo wako Serikalini pamoja na maazimio ya Bunge, ni leo tu nanyamaza, keshokutwa katika mjadala mwingine nitataja nani wako nyuma ya IPTL, nitataja nani wako nyuma ya ufisadi wa SGR ambayo manunuzi ya loti moja yametugharimu hasara “


Ole Sendeka ameongeza kuwa ufisadi uliofanyika, kama fedha zingetolewa majimboni kwenye miradi ya maendeleo Zanzibar tu ingepata gawio la Tsh bilioni 300.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search