banner

Wednesday, August 23, 2017

Wakuu wa Mikoa pokeeni agizo hili la Makamu wa Rais Samia Suluhu

Wakuu wa Mikoa pokeeni agizo hili la Makamu wa Rais Samia Suluhu

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa mikoa wote nchini kuzingatia na kuhakikisha kuwa bilioni 11 zilizotengwa kwa ajili ya watoto kwa kila Halmashauri zinawafikia walengwa na zinatumika kama ilivyopangwa, ili kusaidia watoto kuondokana na matatizo ya utapiamlo yanayotokana na ukosefu wa virutubisho.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kwanza kitaifa la Urutubishaji wa chakula kwa mikoa ya Tanzania na kusema kuna baadhi ya wazazi wamekua wakiwanyima watoto wao haki ya msingi pindi wanapowabaini kuwa na ulemavu.


Katika hatua nyingine Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekemea wazazi na walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu kwa kisingizio cha kuwaletea mikosi kwenye familia na kusema serikali haitawafumbia macho.


"Serikali haitalifumbia macho jambo suala la wazazi wanaoficha watoto wenye ulemavu na tutachukua hatua za haraka za kuwa nusuru watoto hao kwa kuwakamata walezi wao", alisema Mama Samia.



Pamoja na hayo, Makamu wa Rais amewataka watoa huduma za afya washirikiane na wataalam wa lishe ili waweze kuhakikisha wanaboresha huduma ya lishe kwa wazazi na kunusuru wajawazito kujifungua watoto wenye kasoro.



Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia , Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema wanasimamia sera ya afya kwa makini.









Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search