banner

Friday, March 1, 2024

BURIANI MZEE MWINYI

 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Mzee Ali Hassan Mwinyi (98), Rais wa awamu ya pili wa Tanzania.



Mzee Mwinyi amefariki dunia saa 11 jioni ya leo Alhamisi Februari 29,2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


“Kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia leo Februari 29 saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu.


Mzee Ali Hassan Mwinyi, amekuwa akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana huko London, Uingereza na baadaye kurejea nchini na kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena,” amesema Rais Samia.


Mkuu huyo wa nchi amesema, kutokana na kifo hicho, bendera zitapepea nusu mlingoti kwa siku saba kuanzia kesho Ijumaa, Machi 1, 2024.


Mzee Mwinyi amefariki dunia akiwa na miaka 98 na miezi tisa na siku 21. Sawa na siku 36,091.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search