banner

Thursday, September 20, 2018

DC Mjema asema kero zitatatuliwa kwa mikutano

DC Mjema asema kero zitatatuliwa kwa mikutano



MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema kero za Wananchi zitatatululiwa endapo watendaji wa chini wakijenga utamaduni wa kukaa vikao na Wananchi wao.

 Amesema kuwa, katika ziara zake zote alizofanya amegundua kwamba Watendaji hawakai vikao na Wananchi wao jambo ambalo linaweka mrundikano wa kero nyingi ambazo wangeweza kuzitatua wenyewe  bila ya yeye kuhusika.

 Aidha amesema watendaji wanajisahau sana kwani Serikali hii ya awamu ya tano inataka  wananchi wasikilizwe na wapatiwe majibu kikamilifu ili kupiga hatua ya maendeleo.

" Hii ni awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ni kazi tuu, lazima tufuate Ilani ya Chama inavyotaka na kufanya Yale yanayotakiwa na Serikali "Amesema DC Mjema.

Katika hatua nyingine , amezungumzia kero ya Barabara huku akisema Greda  litafika katika maeneo  yenye changamoto na hakuna mwananchi atakae tozwa Pesa.

Akizungumzia kuhusu ulinzi shirikishi , amesema wale wanaolalamikiwa wanatakiwa wafuatwe na kuwajibishwa ili wasichafue Jeshi la  Polisi.

 Kuhusu Msitu wa Nyuki, amesema pamoja na shida kubwa ya watu kukabwa na ujambazi lazima waangalie faida zake kama ni kweli  unawanufaisha Wananchi maana kuna baadhi ya watu wamepanga kupata ardhi kwa makazi.

Kuhusu Jukwaa la  Wakina mama ametaka wajiunge ili kuchangamkia fursa.

Katika suala la  Ulinzi amesema wapo katika mchakato wa kufanya Operesheni ili kuwabaini waharifu ambapo operesheni ya Ukonga itafanyika mwishoni Mwa mwezi wa kumi huku ya Segerea ikitarajiwa kufanyika mwishoni Mwa mwezi wa kumi na moja.  

Naye  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlazi, amesema kupitia ziara hii imesaidia sana Viongozi na kutatua kero za Wananchi.

Amesema DC Mjema, amerahisha kazi kwa watendaji wa chini. " DC Mjema ni mfano wa kuigwa, kama Viongozi wote watafanya hivi nahakika kabisa  kero zitapungua na sisi tutakuwa tunapeleka kero kwao  badala ya wao kuja huku" Amesema Milanzi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search