banner

Thursday, September 20, 2018

Marufuku Mgambo kuingia nyumba za watu na kukagua Vyoo hiyo siyo kazi yenu: DC Mjema

Marufuku Mgambo kuingia nyumba za watu na kukagua Vyoo hiyo siyo kazi yenu: DC Mjema

 MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema Mgambo  hawana mamlaka ya kukagua vyoo na kuingia ndani kwa mtu  kwani wenye  jukumu hilo  ni Bwana Afya na Bibi Afya nasivinginevyo.      

 Amesema kuwa zipo taarifa nyingi  za malalamiko kuhusiana na mgambo kwamba wanawanyanyasa kuwapiga na kuwatoza faini sasa hizo kero hataki kuzisikia.

"Ndugu zangu kazi ya mgambo ni kuwaelekeza Wananchi jinsi ya kufanya usafi na baada ya hapo watakao kaidi walipishwe faini  ila sio wanafika tu wanatoza faini bila kuwapa Elimu ya usafi"amesema DC Mjema.

Amesema suala la  taka taka ni changamoto kwa kuwa wamebakia na magari machache ambapo mengine ni tenda kwa walioomba kufanya usafi hivyo katika kuona suala hilo linafanyiwa kazi wamejipanga kuleta magari 5 yatakayo hudumia Kata ya Gongolamboto, Minazi mirefu, Kiwalani pamoja na kipawa ili kupunguza asilimia 55% ya taka inayobakia mitaani.

Amesema Serikali inampango wa kuhakikisha taka taka zote zinageuka dili kwa kuja na mfumo wa kugeuza taka taka ngumu kufanyiwa cycling na zile nyingine kuchomwa ili. Kupata gesi mbadala.

Mbali na kero za usafi, amezungumzia suala la  ulinzi Shirikishi huku akisema kuwa lazima wananchi watambue umuhimu wa ulinzi shirikishi  na kulipa Pesa walizokuliana ili kuwasaidia wale waliojitolea kuwalinda.

Pia katika hatua nyingine amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa  kumtafuta mkandarasi aliyejenga Mradi wa Maji uliopo Kata ya Minazi mirefu ili alipie gharama hizo za ujenzi upyaa maana mradi haujakizi vigezo na wale wote waliohusika na kukwamisha huo mradi wachukuliwe hatua.

"Mradi huu ni wa muda mrefu sana japo  hizo kero za kukosekana kwa mfumo wa miundombinu lakini bado Nina mashaka na waliohusika sasa Mkurugenzi hakikisha watu Hawa wanapatikana na kutujibu "amesema DC Mjema.

Katika hatua nyingine , Dc Mjema , amemuagiza RPC , kuwakamata wale walio  na makanisa ambayo hawana kibali yafungwe.

Amesema yapo  makanisa yanayopiga mziki masaa 24 hivyo yaache haraka sana tabia hiyo.

" Rpc   nakuagiza kamata wale wote wanaoanzisha makanisa na kufanya ibada SIKU zote za kazi kwa kutumia mziki, huu sio utaratibu Bali tunawatesa wenzetu kuna watu wanahitaji kupumzika watoto wanahitaji kisoma, he watasoma muda gani? Sasa kuanzia Leo tunaanza operesheni ya ukaguzi huo Mara moja ili kuwabaini watu hao" amesema Dc Mjema.

Bar zinazopiga mziki masaa 24 ambazo hazina leseni ziache Mara moja hatua Kali za kisheria zitachukuliwa zidi yao.




Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search