banner

Wednesday, September 26, 2018

DC Mjema kuja na mikakati maalumu ya kuwatambua Wafanyabiashara wa Vingunguti Machinjioni

DC Mjema kuja na mikakati maalumu ya kuwatambua Wafanyabiashara wa Vingunguti Machinjioni

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema yupo katika mipango ya kuhakikisha Wafanyabiashara wote waliopo Machinjioni wanaingia katika Databases ( kumbukumbu za utambuzi).

DC Mjema ameyasema hayo leo kwenye ziara yake  Mara alipotembelea Machinjio hayo ili kuona kero zinazowakabili.

Aidha,  DC Mjema, amesema anataka kuona Wafanyabiashara hao hawapati shida na kunyanyaswa kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano  ipo  kwa ajili yao.

 "Nataka mtembee kifua mbele na kuacha dhana ya kudharauliwa kwani mnategemewa katika Serikali ya Wanyonge" Amesema DC Mjema.

Amesema wakati wanakwenda   kuingia kwenye Machinjio ya kisasa lazima wajue wanakwenda kufanya kazi wapi na vipaumbele vitolewe kwa Wafanyabiashara husika.

Amesema Wafanyabiashara wa Machinjio wanakila sababu ya kuhalalishwa kwakuwa wanachangia pato kubwa katika Manispaa ya Ilala.

Katika hatua nyingine, amesema eneo litakalo jengwa  Machinjio ya kisasa  litakuwa na eneo la  Mita za mraba Elfu Ishirini ambapo Mita 10 za mraba waangalie kutenga eneo la  Wafanyabiashara wa nje wanafuata Nyama.

Akijibu tuhuma za Wakina mama kukaa nje na kulala wakizuiwa kuingia ndani, amesema kuwa kwa sasa ruksa kuingia lakini wafuate kile  walichokifuata.

Akizungumzia kuhusu kuporomoka kwa bei ya ngozi ,amemtaka Kiongozi anayeshikilia idara hiyo ahakikishe mpaka kufikia tarehe 26 mwezi 10 wakae ili kuandaa mpango wa wa semina ya ngozi kwa Wafanyabiashara ili kuona Serikali itaingiza kiasi gani na wao ili kulinda maslahi katika Biashara  zao.

 Kero ya Maji, amesema kesho DAWASA wataenda kuangalia jinsi ya kuwasaidia lakini amewatahadharisha kuhusu uzwaji wa Maji hayo na watakao bainika watachukuliwa hatua.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search