banner

Wednesday, September 26, 2018

Wafanyabiashara mifugo Vingunguti Machinjioni walia na Ushirikishwaji

Wafanyabiashara mifugo Vingunguti Machinjioni walia na Ushirikishwaji

 WAFANYA Biashara ya Mifugo katika Machinjio ya Vingunguti wamelalamikia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh: Sophia Mjema, kutoshirikishwa katika maamuzi juu ya utendaji unaofanyika katika Machinjio hayo.

Wakizungumza na waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti tofauti leo kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya ikiwa ni kutatua kero za Wananchi (Majina yao yamehifadhiwa)  , wamesema kuna mambo ya hovyo yanayofanywa na Watendaji wao hawaridhishiwi nayo kutokana na kutoshirikishwa katika shughuli zinazofanyika katika Machinjio hayo.

Naye , Kaimu Afisa Mfawidhi Machinjio ya Vingunguti, Mgeni Abdallah,  amesema Chinjio hilo linachangamoto sana hivyo wamemuomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuwasaidia kutatua kero zao.

Aidha katika kutoa taarifa fupi ya Machinjio, Mfawidhi Mgeni, amesema Machinjio hayo yalianziashwa 1959 wakiwa na wastani kuchinja Ng'ombe 25-30, na mbuzi.

 Pia amesema kwa sasa wanachinja Ngo'mbe 500 hadi 600 na Kondoo 400 hadi 450 kwa siku ambapo ni tofauti na awali.

" Tunashukuru sana ,Dc Mjema, kwa kuja hapa kutusikiliza sisi bado tupo katika hali mbaya hivyo Machinjo ya kisasa  tunaimani mambo yatakuwa mazuri "Amesema Mgeni.

Aidha katika hotuba yao, wamesema katika mwaka wa bajeti ya mwaka 2015/2016 walikusanya milioni 634,  mwaka 2016/2017 milioni 771 na mwaka 2017 hadi kufikia mwezi Juni 2018 milioni 920.

Katika kuelezea changamoto, amesema idadi kubwa ya watu na baadhi yao wakiwa hawana shughuli maalumu ina  punguza  malengo waliojiwekea.

Pia uwepo wa miundombinu mibovu unachangia kutokuwepo  kwa huduma rafiki kwa wateja.

Aidha amezitaja shughuli mbali mbali wanazozifanya ikiwamo shughuli za ukaguzi wa awali wa Nyama, pamoja na  ukusanyaji wa ushuru wa Machinjio.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search