banner

Wednesday, October 3, 2018

Kumbilamoto aibuka kidedea Naibu Meya Ilala

Kumbilamoto aibuka kidedea Naibu Meya Ilala



UCHAGUZI  wa Naibu Meya Ilala umemalizika huku Omary Kumbilamoto, akiubuka kidedea baada ya kupata kura 27 kati ya kura 52 zilizopigwa.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea watatu walishiriki  kuchukua fomu ambapo Mgombea wa Chadema aliwakilisha Patriki Assenga,  Adam Rajabu Fugame ( CUF).

Katika kura hizo, mgombea wa Chadema Patriki Assenga, amepata kura 0 na Mgombea wa CUF Adam Rajabu Fugame kura 25.

Aidha uchaguzi huo uligubikwa na sintofahamu Mara baada ya Mgombea wa Chadema kujitoa katika kinyang'anyiro hicho na kuungana na Mgombea wa CUF.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, msimamizi wa uchaguzi, Makame Jabiri, amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki kwa kusimamia Sheria zote za uchaguzi.

Amesema kwamba, wamezingatia kanuni na taratibu,  hivyo hakuona sababu za yeye kutomtangaza mshindi licha ya kuwepo kwa madai ya wagombea kutokubaliaba na matokeo.

Naye  Naibu Meya mteule, Omary Kumbilamoto, amewashukuru wote waliompigia kura huku akisema hatawaangusha na kupania kufanya mabadiliko makubwa katika kipindi hiki cha mwaka mmoja kilichobakia.

 Amesema yeye ni muumini wa maendeleo hivyo Yale aliyoyafanya kipindi cha nyuma ataendelea nayo  ili kuhakikisha Manispaa inakuwa salama kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

 " Namshukuru Mungu tumemaliza salama nimeshinda, kilichobakia ni kufanya kazi na kuungana kuwa kitu kimoja uchaguzi umekwisha twendeni tukawatumikie wananchi"amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wa Mgombea wa Chadema, Patrick Assenga, amesema, hajafurahishwa na matokeo kwani wao ndio walistahili kushinda.

 Amesema hawatashiriki tena kwenye uchaguzi, kwani kitendo cha wao kutopewa ushindi kimeonyesha kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi.

" Tumefanyiwa figisu, nasema kitendo walichokifanya ccm , ni kudharirisha chama na kuonyesha ni jinsi gani hawana uwezo mpaka wanatumia nguvu za dola kupora ushindi Sasa tumeamua kususia chaguzi zao kwakuwa hakuna faida za kugombea wakati mshindi anajulikana" amesema  Assenga.

Aidha kwa upande wa Mgombea wa Cuf , Adam Rajabu Fugame, amesema yeye anamaisha yake hivyo kukosa Unaibu Meya hawezi kuumia japo watu wameshinda kwa kutumia nguvu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search