banner

Saturday, November 4, 2023

MIKATABA 15 YA BARABARA KUSAINIWA

MIKATABA 15 YA BARABARA KUSAINIWA




Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) inatarajia kusaini mikataba 15 kwa pamoja ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na daraja zenye thamani ya Sh1.034 trilioni ili kuboresha huduma za miundombinu nchini.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati akitoa majibu ya nyongeza leo Ijumaa Novemba 3, 2023 bungeni jijini Dodoma katika kikao cha nne, mkutano wa 13.


Bashungwa amesema kuwa miradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za miradi ya maendeleo na Serikali iko mbioni kuandaa tukio hilo.


@innocentbash #mo7newsupdates

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search