banner

Friday, November 3, 2023

PICHA YA ASKARI ILIYOZUA MJADALA MTANDAONI

PICHA YA ASKARI ILIYOZUA MJADALA MTANDAONI

 Arizbeth Dionicio Ambrosio alikuwa akifanya kazi ya uokoaji katika mji wa Acapulco nchini Mexico baada ya uharibifu uliosababishwa na kimbunga Otis, aliposikia mtoto akilia kwa mbali.


Baadaye kidogo, afisa huyo wa polisi mwenye umri wa miaka 33 na mama wa watoto wawili alisikia kilio hicho tena na kuamua kuchunguza kilitokea wapi.

Hapo ndipo alipokutana na mama wa mtoto wa miezi minne ambaye alihitaji msaada. Mama alimwambia mwanae hakuwa amepata chakula kwa zaidi ya siku mbili na alikuwa akilia kwa sababu ya njaa.

"Nilimwambia kwamba ikiwa, kwa vile ninanyonyesha, kama angetaka ningeweza kumpa," afisa huyo aliambia mtandao wa N+ wa Mexico.

Polisi huyo alivua zana zake za usalama na kuanza kumnyonyesha mtoto mwenye njaa, ambaye aliacha kulia haraka.

"Ni hisia nzuri . Ni mtoto - ikiwa kuna jambo moja ambalo linatuumiza kama akina mama, ni kuona mtoto katika mazingira haya," Dionicio alisema.

Hatua hiyo ilinaswa katika picha iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Sekretarieti ya Usalama wa Raia (SSC) ya Mexico City, ambayo ilituma timu za uokoaji Acapulco.

Picha hizo ziliibua hisia za kuungwa mkono kwenye mitandao ya kijamii, katikati ya maafa ambayo Acapulco inakumbana nayo baada ya kimbunga hicho kupita.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search