banner

Friday, November 3, 2023

WABUNGE WAKATAA OMBI LA SERIKALI KUNUNUA BOTI YA KIFAHARI KWAAJILI YA RAIS

WABUNGE WAKATAA OMBI LA SERIKALI KUNUNUA BOTI YA KIFAHARI KWAAJILI YA RAIS



Wabunge hao wamesema Bunge haliwezi kuidhinisha kiasi hicho cha Fedha kwasababu ni matumizi mbaya ya Kodi za Wananchi hasa kwa kipindi ambacho Nchi inakabiliwa na mdororo mkubwa wa Uchumi



Serikali ya Rais #BolaTinubu imeanza kukumbana na changamoto tangu kuingia kwake madarakani ambapo Mwezi Oktoba 2023, Bunge lilipitisha Bajeti ya Serikali ya Tsh. Trilioni 132.3 huku ikiwa na Fungu la Tsh. Bilioni 89.9 kwaajili ya Matumizi ya Ikulu ikiwemo kununua Magari ya Kifahari na ukarabati wa Ofisi ya Rais



Matumizi mengine ni pamoja ununuzi wa Ndege mpya ya Rais Tsh. Bilioni 37.4. Wabunge wamesema Bunge haliwezi kupitisha Bajeti ya kununua Boti wakati zaidi ya Wananchi Milioni 137 wanaishi kwenye umasikini uliokithiri huku Mfumuko wa Bei za Bidhaa ukiwa ni 26.7% hadi kufikia Septemba 2023

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search